Uharibifu uliosababishwa na kimbunga Debbie nchini Australia

Lismore huku New South Wales iliathirika vibaya Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lismore huku New South Wales iliathirika vibaya

Australia inakadiria uharibifu uliosababishwa na kimbunga Debie, ambacho kilisababisha mafuriko eneo kubwa, sawa na jimbo la Texas.

Kwa sasa kibunga hicho kimeelekea bahari ya Tesman, baada ya kusababisha mvua pwani ya mashariki kilipopita jimbo la Queensland.

Tisho la kutokea mafuriko bado lipo. mimea imezama na hasara inaweza kufika mamilioni ya dola.

Mwili wa tatu ulipatikana huko Queensland Jumamosi jioni.

Mtu mwenye umri wa miaka 77 naye alifariki kutokana na mafuriko huko Logan.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Visiwa vya Whitsunday vilikuwa karibu na eneo kimbunga hicho kilitua

Watu wengine kadha hawajulikani waliko.

Kuna hofu kuwa eneo la Rockhampton, kati kati mwa Qeensland, linaweza kukumbwa na mafuriko mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 60 iliyopita

Jeshi na watoa huduma za dharura wanajikakamua kurejesha huduma za maji na umeme katika maneo yaliayothiriwa.

Maelfu ya watu wamelazimika kuhama makwao.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Visiwa vya Whitsunday vilikuwa karibu na eneo kimbunga hicho kilitua
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mafuriko huko Lismore