Mali yatakiwa kuzungumza na waasi, kaskazini mwa nchi

Asakari wa Ufaransa wakiimarisha ulinzi nchini Mali Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Asakari wa Ufaransa wakiimarisha ulinzi nchini Mali

Serikali ya Mali imetakiwa kuanzisha mazungumzo na waasi wa kiislamu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na wajumbe katika mkutano ulioandaliwa kusaidia kufikia kwa maridhiano ya kitaifa na kuanza kutumika kwa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2015.

Wapiganaji wa Kijihad ambao walishindwa kusaini makubaliano ya amani wamekuwa wakiendelea kuleta ghasia kaskazini mwa Mali.

Kundi hilo likiongozwa na raia wa Algeria Mokhtar Belmokhtar limesema limeua watu sitini tangu kuanza kwa mwezi Januari mwaka huu katika mashambulio ya kujitoa mhanga kwenye kambi za jeshi.