Mgomo kutishia biashara ya mafuta Nigeria

Muhammadu Buhari alikuwa Kiongozi mwenye dhamana na sekta ya mafuta Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muhammadu Buhari alikuwa Kiongozi mwenye dhamana na sekta ya mafuta

Madereva wa Malori yanayobeba mafuta nchini Nigeria wanatarajiwa kuwa na mgomo siku ya Jumatatu.

Chama cha wafanyakazi wa Petroli na Gesi asili nchini humo kimesema watagoma kupinga mishahara midogo na barabara mbovu ambazo zinaharibu magari yao.

Msemaji wa chama cha wafanyakazi, Cogent Ojobo, ameonya kutokea kwa upungufu wa Petroli, Dizeli na mafuta ya taa nchi nzima wakati huu ambapo usambazaji utasitishwa.

Ojobo amesema hakuna tarehe ya mwisho wa mgomo iliyoelezwa