Mkwewe Trump, Kushner anatarajiwa kuizuru rasmi Iraq

Jared Kushner na mkewe Ivanka Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jared Kushner na mkewe Ivanka Trump

Mkwewe Donald Trump ambaye pia ni mshauri mkuu wa Ikulu ya Marekani, Jared Kushner, anafanya ziara rasmi nchini Iraq.

Afisa mmoja wa utawala wa Trump amethibitisha kuwa Kushner anasafiri na Jenerali Joseph Dunford, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi ya Marekani.

Dhamira ya ziara hiyo haijabainishwa wazi.

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amekutana na rais Trump kwa mara ya kwanza tarehe 20 mwezi Machi.

Mada zinazohusiana