Mgomo utaathiri biashara ya mafuta Nigeria

Mwanamume anajaza mafuta kwenye gari Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgomo huo unatishia kuwaathiri mamilioni ya watu iwapo makubaliano hayatofikiwa

Madereva wa magari ya kubeba mafuta wamegoma nchini Nigeria.

Wanachama wa mojawapo ya vyama viwili vikuu vya biashara ya mafuta wanalalamika kuhusu malipo duni na hali mbaya ya barabara nchini.

Mgomo huo wa muda usiojulikana unatishia kuwaathiri mamilioni ya watu iwapo makubaliano hayatofikiwa.

Viongozi wa chama hicho cha wafanyakazi wanasema vituo vya mafuta vitafungwa jambo litakalosababisha upungufu wa petroli, dizeli na mafuta ya taa.

Madereva wa magari hayo ya mafuta ambao ni wanachama wa chama cha wafanyakazi wa mafuta na gesi Nigeria - wanalalamika kuhusu hali duni za utendaji kazi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Nigeria nimojawapo ya mataifa ya frika yanayozalisha mafuta pakubwa

Afisa mkuu wa chama cha wafanyakazi ameiambia BBC kwamba mazungumzo yanaendelea katika mji mkuu Abuja yanayonuiwa kumaliza mgomo huo.

Mgomo huo ulitangazwa wiki iliopita baada ya chama cha wafanyakazi na serikali kushindwa kufikia makubaliano.

Ukosefu wa mafuta ni jambo la kawaida Nigeria.

Mwaka jana mzozo kuhusu bei ya mafuta ulisababisha msongamano na misururu mirefu katika vituo vya kuuza mafuta kwa wiki kadhaa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii