Nguo zinazoshonwa kwa kutumia miti Burundi
Huwezi kusikiliza tena

Annick Kabates anatumia miti kutengeneza vitambaa na kuwashonea wateja nguo

Ubunifu umekuwa ukiongezeka kila siku, mjini Bujumbura Mwanzilishi wa shirika linalotengeneza nguo kutokana na magome ya miti, Annick Kabates amekuwa akitumia miti aina ya fucus kutengeneza vitambaa na hatimaye nguo kwa wateja.

Nguo wanazotengeneza hupelekwa katika maonesho mbalimbali barani Afrika. Ndoto yake, ni shirika kupanda kwa wingi miti kama malighafi ili kutengeneza nguo nyingi na kupata fedha zaidi.

Ismail Misigaro alizungumza naye