Polisi wawapiga risasi na kuwaua mifugo wengi Kenya

Polisi wawaua mifugo wengi nchini Kenya kwa kuwapiga risasi
Image caption Polisi wawaua mifugo wengi nchini Kenya kwa kuwapiga risasi

Ripoti ya kutoa kituo cha televisheni cha NTV cha nchini Kenya zinasema kuwa maafisa wa usalama waliotumwa eneo la Laikipia kufuatia uvamizi ulitokea katika mashamba ya kibinafsi na mahoteli uliofanya na wafugaji, wamekuwa wakiwaua kwa kuwapiga risasi mifugo wanaomilikiwa na jamii za wafugaji

Awali mamlaka zilikana madai kuwa polisi wamekuwa wakiwaua mifugo kulipiza uvamizi wa wafugaji hao.

Ukame unaoendelea kushuhudiwa unaripotiwa kuwalazimu wafugaji kutafuta malisho kwenye mashamba ya kibinafsi, lakini baadhi yao wameripotiwa kupora na kuchoma moto hoteli za kibinafsi.

Mmoja wa wafugaji aliyehojiwa alisema kuwa polisi waliwaua mifugo wake kwa kuwapiga risasi.

Image caption Ukame unaoendelea kushuhudiwa unaripotiwa kuwalazimu wafugaji kutafuta malisho kwenye mashamba ya kibinafsi