Waziri mkuu wa Canada kupigana ndondi na mcheza filamu

Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akiwa kwenye Mazoezi mwaka 2012 Haki miliki ya picha God Save Justin Trudeau, Productions de la Ruelle
Image caption Waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau akiwa kwenye Mazoezi mwaka 2012

Katika historia ya masumbwi ni majina machache yaliyo maarufu

Muhammad Ali na Joe Frazier. Evander Holyfield na Mike Tyson. Sugar Ray Leonard na Tommy Hearns.

Na sasa pambano linalokuja ni kati ya Matthew Perry na Justin Trudeau.

Mcheza filamu Matthew Perry na waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau, wamesema kuwa huenda wakapimana nguvu baada ya bwana Tradeau kutaka pigano lilofanyika shuleni miaka 35 iliyopita kurudiwa.

Ujumbe ambao Trudeau aliandika kwenye mtandao wa Twitter tarehe mosi mwezi Aprili, ulikuja baada ya bwana Petty kukiri kuwa wakati mmoja alimtandika bwana Trudeau.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe kutoka kwa Justin Trudeau

Perry aliakiambia kituo kimoja cha runinga cha Marekani kuwa wote walikuwa shule moja ya msingi huko Ottawa, wakati yeye na rafiki wake waliamua kumpiga kijana huyo mdogo.

"Nafikiri alikuwa mtoto peke yake ambaye nilikuwa na uwezo kumpiga," Perry alisema.

Mambo hata hivyo yamebadilika miaka iliyopita. Perry amekuwa mmoja wa watu maarufu katika sekta ya filamu duniani.

Naye bawana Trudeau ambaye anataja ndondi kama mchezo anaoupenda amefuata nyayo za babake na kuwa waziri mkuu wa Canada.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe kutoka kwa Matthew Perry