Raia waliokwama kuondoshwa mjini Mosul

Raia laki nne wamekwama mjini Mosul kutokana na mashambulizi yanayoendelea Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia laki nne wamekwama mjini Mosul kutokana na mashambulizi yanayoendelea

Vikosi vya Iraq vimefungua njia ya kuwawezesha raia waliokwama kutokana na mapambano mjini Mosul kupata upenyo wa kukimbia mapambano yanayoendelea ya kuwatoa wapiganaji wa IS kwenye eneo la mwisho wanalolidhibiti.

Kamanda mjkuu amesema njia hizo zimelenga kuruhusu mchakato wa kuwaondoa raia kabla Serikali ya Iraqi haijafanya shambulizi kubwa ili kudhibiti eneo hilo.

Raia laki nne wanakisiwa kubaki katika sehemu ya eneo la mji wa Mosul.

Kumekuwa na taarifa za raia kuathiriwa vibaya kutokana na mashambulizi yanayotekelezwa na Serikali, yakisaidiwa na mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na vikosi vya Marekani