Colombia yatangaza hali ya dharura baada ya maporomoko ya ardhi

Wanaume wanalia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Manusura wa maporomoko ya Jumamosi wameanza kuwazika jamaa zao

Rais wa Colombia ametangaza hali ya dharura kiuchumi kijamii na ki mazingira wakati wahanga wa kwanza wa maporomoko ya ardhi huko Mocoa wakizikwa.

Juan Manuel Santos amesema serikali inakusanya $ milioni 13.9 zitakazosaidia kukabiliana an masuala ya kibinaadamu.

Wakati huo huo mazishi ya kwanza ya wahanga 262 waliouawa katika maporomoko ya Jumamosi yamefanyika.

Lakini bado jitihada za kutafuta manusura zinaendelea.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Athari ya maporomoko Mocoa

Shirika la msalaba mwekundu limeliambia shirika la habari la AFP kwamba bado wana muda katika saa 72 za kwanza baada ya mkasa na wanatumai kupata manusura. Hatahivyo matumaini yanafifia miongoni mwa wakaazi wanaotafuta jamaa zao waliosombwa katika udongo, mawe na kifusi vinavyotokana na maporomoko hayo yalioukumba mji huo uliopo kusini magharibi mapema Jumamosi.

Wanaosalia bado wanasubiri usaidizi wa kibinaadamu.

Rais Santos ameahidi uwekezaji zaidi katika mji wa Mocoa zaidi ya ilivyokuwa awali, na kumkabidhi mamlaka waziri wa ulinzi Luis Carlos Villegas kuusimamia mji huo.

Lakini wakosoaji wa rais Santos wanasema hatua zaidi zingechukuliwa kulilinda eneo hilo kutokanana majanga kama hayo.