Eritrea yapinga vikwazo vya Marekani

Mwanajeshi akifanya mawasiliana na wenzake
Image caption Mwanajeshi akiwasiliana na wenzake

Eritrea imepinga vikwazo ilivyowekewa na Marekani kwa kufanya biashara ya vifaa vya kijeshi na Korea kaskazini.

Mpango huo ulibainika katika ripoti ya kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya 2016 iliotolewa mnamo mwezi Februari, ambapo masanduku 45 ya vifaa vya kijeshi vya mawasiliano vilipatikana vikielekea Eritrea kutoka North Korea.

Eritrea imepinga matokeo ya ripoti hiyo

Mamlaka za Asmara zimeonekana kujibu hatua za Marekani na kuzilaani vikali.

Eritrea yapinga vikwazo vya Marekani

Taarifa kutoka wizara ya habari zimesema kwamba hatua ya Marekani siyo ya haki na kwamba haifai kabisa.

Asmara imeongeza kwamba sera ya Marekani kwa nchi hiyo ni ya kupotosha na kwamba hatua hii inaambatana na vikwazo vya Umoja wa Mataifa vilivyotarajiwa kujadiliwa upya mwezi huu.

Marekani huwekea vikwazo kwa taifa lolote ambalo huweka mikataba ya kijeshi na Iran, Korea Kaskazini na Syria.

Vikwazo vya sasa vimelenga jeshi la wanamaji la Eriterea pamoja na jeshi la Sudan.

Hii inamaana kwamba serikali ya Marekani haiwezi kufanya biashara yeyote au kutoa msaada wowote kwa matafa yaliyowekwa kwenye orodha hiyo.