Wafanyikazi 4 wa misaada watekwa nyara Mogadishu

Ramani ya taifa la Somalia ambapo wafanyikazi 4 wa shirika la afya duniani WHO wametekwa nyara
Image caption Ramani ya taifa la Somalia ambapo wafanyikazi 4 wa shirika la afya duniani WHO wametekwa nyara

Wafanyi kazi wanne wa shirika la utoaji misaada nchini Somalia, wametekwa nyara katika eneo la Gedo, kaskazini magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.

Wanne hao walikuwa wakifanya kazi na shirika la Afya Duniani WHO, katika mji wa Luq, kwenye kampeini ya kupambana na ugonjwa wa polio.

Duru zasema kuwa walitekwa na wanamgambo wa Al Shabaab, lakini taarifa hiyo bado hazijathibitishwa.

Eneo la Gedo, limeathirika pakubwa na ukame, na ni mojawapo ya maeneo ambayo wapiganaji wa al-Shabaab, wanadai kwamba wanawapa chakula cha msaada watu walioathirika na ukame huo.