Lazio yatinga fainali ya Copa Italia

Copa italia Haki miliki ya picha Google
Image caption Winga wa As Roma Mohamed katikati akiwatoka wamchezaji wa Lazio

klabu ya Lazio imetinga katika hatua ya fainali ya kombe la Copa italia licha ya kuchapwa na As Roma kwa 3-2 katika mchezo wa nusu fainali ya pili.

katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza Lazio walishinda kwa mabao 2-0. Hivyo wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3.

Roma walipata mabao ya kupitia kwa Stephan El Shaarawy katika dakika ya 44, kisha Mohamed Salah akaongeza mengine mawili katika dakika ya 66 na 90.

Mabao ya Lazio yalifungwa na kiungo Sergej Milinkovic-Savic na bao la pili likifungwa na mshambuliaji Ciro Immobile

Nusu fainali ya pili ya kombe la Copa itapigwa leo kwa Napoli kuwaalika Juventus dimba la San Paolo