UN yaikosoa Marekani kuondoa mfuko wa fedha wa kusaidia masuala ya afya ya uzazi duniani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Antonio Guterres

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amekosoa uamuzi wa Marekani wa kuondoa fungu la pesa kutoka kwenye mfuko wa umoja wa mataifa unaoshughulikia idadi ya watu uliokuwa ukisaidia masuala ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango duniani.

Antonio Guterres amesema kupoteza pesa hizo takriban dola milioni thelathini na mbili mwaka huu pekee, kunaweza kuleta madhara makubwa kwa afya za wanawake na watoto wanaohitaji msaada.

Wizara ya mambo ya nje imesema inasitisha uchangiaji kwenye mfuko huo kwa sababu shirika hio linaunga mkono programu ya china ya utoaji mimba.

Taasisi hiyo ya umoja wa mataifa imesema haiungi mkono wala kusaidia vitendo vya utoaji mimba, pia haijavunja sheria yeyote ya Marekani.