Urusi: silaha za kemikali zilizowaua watu Syria ni za waasi

watoto Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto wengi kutajwa kuathirika zaidi

Urusi inasema kuwa shambulizi la gesi ya kemikali ambalo liliwaua na kuwajeruhi watu kadha katika mji unaodhibitiwa na waasi kaskazini mwa Syria lilitekelezwa na silaha za waasi.

Wizara ya ulinzi nchini Urusi ilikiri kuwa ndege za jeshi la Syria zilishambulia mji wa Khan Sheikhounulio ulio mkoa wa Idblib.

Lakini hata hivyo iliseme akwa ndege hizo zilishambulia ghala linalotumiwa kutengeneza milipuko lenye kemikali za sumu.

Marekani na nchi zingine zinasema kuwa ndege za Syria ndiza ziliangusha silaha za kemikali madai ambayo Syria iliyakanusha

Naye waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uingerea, alisema kuwa kuna ushahidi unaoonyesha kuwa shambulizi hilo lilifanywa na utawala wa rais Bashar Assad.

Jumuiya ya kimataifa imelaani shambulio huku shirika la kimataifa linalopambana na matumizi ya silaha za kemikali OPCW limesema linakusanya ushahidi.

Naye mkuu wa sera za mambo ya nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini amesema pande zote na wadau kwenye vita ya Syria wanatakiwa kupata suluhu ya kisiasa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zahati ni miongoni mwa sehemu zililengwa katika shambulio hilo

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano kuhusu mustakabali wa Syria, Mogherini amesema EU inategemea kila mmoja kutimiza wajibu wake kumaliza vitendo vya umwagaji damu.

''sisi Umoja wa Ulaya, si tunaotekeleza mashambulizi, sisi si tunaopigana, sisi ndio tunaotoa misaada ya kibinaadam, kuusaidia Umoja wa mataifa kufikia makubaliano na suluhu ya kisiasa na sisi ndio tunaokuwa tayari kuwasaidia raia wa Syria kujenga mustakabali wao kwa ajili ya taifa lao, hii ndio njia tunayotumia, hii ndio namna tunavyoamini sera ya nje inavyopaswa kutekelezwa, na tunasisitiza hilo, lakini haimaanishi kuwa mtu aharibu kila kitu kisha tulipe gharama. hili kamwe haliwezi kutokea'' alieleza

Kufuatia shambulio la anga jimboni Idlib kulitolewa ripoti zikisema kuwa mamia ya watu hasa watoto walikuwa wakitapika, kupaliwa na kutoja povu mdomoni

Serikali ya Marekani imesema shambulio lililotekelezwa Syria ni la kukemewa. Msemaji wa Serikali Sean Spicer ameinyooshea kidole serikali ya Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuhusika na mashambulizi hayo.

Syria imekana kutumia silaha za kemikali.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura siku ya Jumatano kujadili shambulizi hilo