Korea Kaskazini yafyatua kombora kuenda bahari ya Japan

korea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption kombora lililorushwa na Korea Kaskazini

Japan imeijibu vikali Korea Kaskazini kufuatia nchi hiyo kufyatua kombora jingine hivi karibuni na kutaja hilo ni tatizo kubwa lililopindukia.

Katika Mji wa Pyongyang,Kombora lenye uzito wa kati lilirushwa upande wa mashariki mwa bandari ya Sinpo kuelekea bahari ya Japan.

Waziri kiongozi wa nchi hiyo ,Yoshihide Suga amewaambia waandishi wa habari kuwa nchi yake haiwezi stahimili vitendo hivyo vya uchochezi ambavyo Korea kaskazini imevirudia kuvifanya.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Korea Kaskazini kurejea kurusha makombora Japan

Kombora hilo limerushwa siku chache kabla ya rais wa China, Xi Jinping kufanya ziara nchini Marekani kukutana na rais Trump ili kujadili namna ya kudhibiti mipango ya Nuklia na makombora ya masafa marefu ya Korea kaskazini. .