Bei ya mafuta yaongezeka Tanzania

Tanzania Haki miliki ya picha Google
Image caption Bei ya mafuta yapaa Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa zitakazoaanza kutumika kuanzia leo.

Akitangaza bei hizo leo Meneja wa Mawasiliano wa Ewura nchini Tanzania , Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 na itauzwa kwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.

"Mabadiliko haya bei yametokana na bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita,"amesema Kaguo.