Mbwa amzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga Nigeria

Mbwa amzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga Nigeria Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mbwa amzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga Nigeria

Mbwa mmoja aliokoa maisha ya watu wengi wakati ya sherehe ya harusi mjini Maiduguri nchini Nigeria, kwa kushambulia mwanamke moja mshambuliaji wa kujitoa mhanga.

Inaarifiwa kuwa mwanamke huyo alijaribu kuingia katika sherehe hiyo ya harusi, kwa mujibu wa kituo cha redio cha jeshi.

Mbwa huyo pamoja na mshambuliaji wa kujitoa mhanga wote walikufa wakati msichana huyo alilipua bomu alipokuwa akimkimbia mbwa huyo.

Polisi wanasema kuwa mbwa huyo alimilikiwa na mwenyeji ambapo wa eneo mabapo sherehe hiyo ya harusi ilikuwa ikifanyika.

Haki miliki ya picha Google
Image caption Mbwa amzuia mshambuliaji wa kujitoa mhanga Nigeria