Mlipuko wa fataki wawaua watu 5 Ureno

Mlipuo wa fataki wawaua watu 5 Ureno
Image caption Mlipuo wa fataki wawaua watu 5 Ureno

Watu Watano wameuawa na wengine watatu wakiwa hawajulikani waliko baada ya mlipuko wa siku ya Jumanne jioni, ulioharibu kiwanda cha kutengeneza fataki karibu na mji wa Lamego nchini Ureno

Wote walionusurika walikuwa wafanyikazi katika kiwanda hicho ambachoo kipo umbali wa kilomita 100 mashariki mwa mji wa Porto.

Mmiliki wa kiwanda hicho alikuwa kati ya walionusurika.

Kiwanda hicho kilitajwa kama biashara ya familia huku meya wa mji huoo akitaja tukio hilo kama la kusikitisha..

Wengi wa walionusurika walitajwa kutoka kwa familia moja.

Baadhi ya walionusurika walipatikana hatua chache kutoka kwa kiwanda, wakiwa wamerushwa kutoka kwa mjengo kufutia nguvu za mlipuko huo.

Maafisa mwanzoni walishindwa kuingia katika majengo kutokana na tahadhari ya usalama wao, televisheni ya umma ilisema