Chanjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria

Chonjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria Haki miliki ya picha EPA
Image caption Chonjo kubwa dhidi ya homa ya uti wa mgongo yaanza kutolewa Nigeria

Watoa huduma za afya nchini Nigeria wameanza shughuli ya kutoa chanjo dhdi ya homa ya uti wa mgongo.

Zaidi ya watu 300 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu mwaka uliopita.

Watoa huduma za afya wanalenga zaidi jimbo la kaskazin magharibi la Zamfara, ambalo ndilo kitovu cha mlipuo wa ugonjwa huo.

Idara ya kukabiliana an magonjwa nchini Nigeria inasema kuwa chanjo 500,000 zilitatolewa.

Maafisa wa afya wanasema kuwa karibu watu 3000 wanashukiwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Hadi sasa watu walioathirika zaidi ni watoto walio kati ya umri wa miaka 5 na 14.

Afisa mmoja aliiambia BBC kuwa jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo zimetatizwa na uhaba wa dawa za kutoa chanjo.