Rais Zuma aponea shinikizo za kumtaka ajiuzulu

Zuma aponea shinikizo za kumtaka ajiuzulu Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zuma aponea shinikizo za kumtaka ajiuzulu

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameungwa mkono na kitengo muhimu cha kutoa umuzi katika chama kinachotawala cha ANC.

Kitengo hicho kilikua kinatathmini malalamiko kutoka kwa maafisa wa vyeo vya juu wa ANC, kuwa Jacob Zuma hakuwaomba ushauri wao wakatia wa mabadiliko kwenye baraza la mawaziri.

Baada ya kuyatathmini malalamiko hayo, ANC imeamu kuwa haitashinikiza kujiuzulu kwa bwana Zuma, kwa mujibu wa maafisa wa chama.

Bwana Zuma amekuwa akikumbwa na shinikizo kali tangu amfute kazi waziri wa fedha aliyekuwa akiheshimiwa Pravin Gordhan.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji mjini Pretoria

Bwana Gordhan alifutwa kazi kama sehemu ya mabadiliko makubwa katika baraza la mawaziri ambayo yalisababisha maswali kutoka kwa uongozi wa ANC ikiwa Zuma atasalia kuwa rais.

Washirika wakubwa wa ANC kikiwemo chama cha SACP na cha Cosatu, walijiunga katika wito wa kumtaka Zuma ajiuzuku.

Lakini kamati iliyokuwa ikijadili suala la mabadiliko ya baraza la mawaziri ya NWC imemuunga mkono Zuma.

Kamati ya NWC ndiyo ya pili kwa utoaji wa maamuzi katika chama cha ANC.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri wa fedha aliyeachishwa kazi Pravin Gordhan