Chelsea yaichapa Man City

EPL Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard akifunga goli la kwanza la Chelsea

Vinara wa ligi kuu ya England, Chelsea wamendeleza wimbi la ushindi katika ligi hiyo baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Stanford Bridge.

Chelsea walipata mabao yao yote mawili kupitia winga wao mahiri Eden Hazard, huku bao la Man City likifungwa na Sergio Aguero.

Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate waliwachapa West Ham kwa mabao 3-0 na hivyo Arsenal kurejea katika nafasi ya tano.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wachezaji wa Arsenal Theo Walcot na Mesut Ozil wakishangilia goli

Liverpool wakashindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kukubalia sare ya mabao ya 2-2 na AFC Bournemouth, Hull City wao wakashinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Middlesbrough.

Tottenham Hotspur wakicheza ugenini katika dimba la Libery waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea City, Southampton wakashinda kwa 3 - 1 dhidi ya Crystal Palace.