Juventus yaifuata Lazio fainali

Coppa Italia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mfungaji wa mabao yoye mawili ya Juventus Gonzalo Higuain akishangilia

Vibibi vizee vya Turin Juventus wametinga fainali ya kombe Copa italia licha ya kufungwa na Napoli kwa mabao 3-2, katika mchezo wa nusu fainali ya pili.

Juventus wamesonga mbele kwa jumla ya mabao 5-4, baada ya nusu fainali ya kwanza kushinda kwa mabao 3-1.

Mchezo wa fainali utawakutanisha Juventus na Lazio na mchezo huo utapigwa june 2 mwaka huu. Katika dimba la Olimpico.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dries Mertens mfungaji wa bao moja la Napoli

Mshambuliajia wa Juventus raia wa Argentina Gonzalo Higuain ndie aliyefunga mabao yote mawili kwa timu yake huku mabao ya Napoli yakifungwa na mshambuliaji Marek Hamsik, Dries Mertens akifunga bao la pili huku Lorenzo Insigneakifunga bao la tatu.