Trump: Mtazamo wangu dhidi ya Rais Assad na Syria umebadilika sana

syria Haki miliki ya picha Google
Image caption Rais wa Marekani Donald Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amelielezea shambulio la kuhusisha gesi yenye kemikali zenye sumu dhidi ya watu wakati wa mashambulizi ya anga kaskazini mwa Syria kuwa ni tukio lisilo la kibinaadamu.

Marekani na mataifa mengine ya magharibi yamemshutumu Rais wa Syria, Bashar Assad na serikali yake kwa kile walichodai shambulio la kutumia silaha za kemikali la siku ya jumanne mjini Khan Sheikhoun.

Trump amesema vifo vya watoto vimebadili mtazamo wake kwa Assad.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption mtoto aliyeathirika katika shambulio la kemikali

''na nitakueleza, kuwa shambulio lile dhidi ya watoto limenifanya niwe na mtazamo mwingine. Ni kitu cha kutisha inatisha sana, na nimekuwa nikifuatilia na kutazama, hakuna namna nyingine zaidi naweza kusema, imekwishatokea kuwa sasa mtazamo wangu kwa Syria na Assad umebadilika sana.''

Marekani, Uingereza na Ufaransa, zote zimemshutumu mshirika wa Serikali ya Syria kwa kile kilichotoka katika mji wa Khan Sheikhoun.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson ambaye anatarajiwa kufanya ziara mjini Moscow nchini Urusi juma lijalo, ameitaka Urusi ifikiri kwa makini kuhusu uhusiano wake na Syria

Image caption Shambulio la kemikali,Syria

hakuna shaka yeyote kuwa utawala wa Syria chini ya Bashar Al Assad unahusika na shambulio hili la kinyama na tunaona sasa ni wasaa kwa warusi kufikiri kwa makinni kwelikweli kuhusu kuendelea kuunga mkono utawala wa Assad''

Urusi imepinga msimamo wa marekani na mataifa ya magharibi kuhusu tukio hilo na kusema kuwa , mswada kuhusu azimio la baraza la usalama la umoja wa mataifa kuhusu shambulio hilo ni chuki dhidi ya Syria.