Mtu na mkewe washinda bahati nasibu kwa mara ya tatu

Mtu na mkewe washinda bahati na sibu kwa mara ya tatu Haki miliki ya picha Western Canada Lottery Corporation
Image caption Mtu na mkewe washinda bahati na sibu kwa mara ya tatu

Mwaka wa 1989 ulikuwa mara ya kwanza kwa Barbara na Douglas Fink kutoka Canada kushinda mchezo wa bahati nasibu na walipata dola 128,000.

Mwaka wa 2010 walishinda dola 100,000. Ushindi wao wa hivi punde wa dola za Marekani milioni 6.1, ndio wao mkubwa zaidi.

Wanandoa hao kutoka Edmonton, Alberta wanasema watatumia pesa hizi kukimu mahitaji ya wana wao na wajukuu .

"Familia ndio muhimu," Barbara aliwaeleza waratibu wa amichezo hiyo. "Tunataka kuhakikisha kuwa watoto wetu wa kike na watoto wao wako sawa."

Douglas anasema pia watatumia kiasi cha pesa hizo kusafiri na baadaye kununua nyumba.

"Barbara anataka nyumba mpya, na ataipata." Alieleza shirika la michezo ya bahati nasibu ya Western Canada Lottery

Ni wao tu na mtu mwingine mmoja ambao waliweza kukisia kikamilifu nambari zote sita zinazohitajika ili kushinda mchezo huu.

Barbara anasema ni yeye aliyegundua kuwa wao ni washindi, mumewe akiwa kazini katika mji mwingine.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii