Shambulizi la kugongwa na gari lamuua mtu mmoja Israel

Shambulizi la kugongwa na gari lamuua mtu mmoja Israel Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shambulizi la kugongwa na gari lamuua mtu mmoja Israel

Raia mmoja wa Israel ameuawa na mwingine kujeruhiwa katika shambuulizi la kugongwa kwa kutumia gari eneo la ukingo wa magharibi, kwa mujibu wa jeshi la Israel.

Jeshi lilisema kuwa dereza wa gari hilo alikamatwa baada ya kisa hicho kilichotokea karibu na makao ya walowezi wa kiyahudi huko Ofra.

Inafikisha 41, idadi ya raia wa Israel waliouawa kwa visu, risasi na kugongwa kwa kutumia magari tangu Oktoba mwaka 2015.

Jeshi halikutoa taarifa zaidi kuhusu mshukiwa, lakini picha zilionyesha kuwa gari hilo lilikuwa na namba za kipalestina.

Walioshuhudia walivyambia vyombo vya habari nchini Israeli kuwa gari hilo lilikaribia kituo cha basi, na kisha likavurumisha kuenda kwa watu wawili waliokuwa wakisubiri basi.

Mwishoni mwa mwaka 2015 na 2016, mashambulizi kama hayo yaliyoendeshwa na Wapalestina au waisrael wenye asili ya kiarabu yalitokea karibu kila siku lakini visa hivyo vimeshuka miezi ya hivi karibuni.

Takriban Wapalestina 242 , 162 kati yao wanaripotiwa kuuwa katia kipindi hicho.