Watoa misaada wanne watekwa nyara Somalia

Watu wenye silaha wamewateka nyara wafanya kazi watano wa kutoa huduma za misaada katika mji wa Beledweyne nchini Somalia.
Wafanya kazi hao ambao wamo wawili wa kujitolea, muuguzi, dereva na daktari wa mifugo walikuwa wakifanya kazi na chama cha madaktari wa mifugo kwa mujibu wa shirika la kibinafsi la habari, Jowhar.
Wafanya kazi waliotekwa walisema kuwa walikuwa wakishiriki kwenye mpango wa utoaji chanjo kilomita 10 kutoka mji wa Beledweye.
Hakuna kundi lililodai kuhusika katika utekaji nyara huo, lakini kundi la wanamgambo la al-Shabab, limeendesha mashambulizi eno hilo awali.
- Maharamia wanadai fedha kuachia Meli
- Maharamia waiteka meli huko Somalia
- Maharamia waiachia huru meli Somalia
Utekaji nyara huo unakuja siku moja baada ya kundi la al-Shabab kuwaachilia watoa huduma za misaada wanne, waliokuwa wakifanya kazi iliyokuwa imefadhiliwa na shirika la chakla duniani WHO, kwenye mji ulio kusini magharibi wa Luuq.