Jesse asaini mkataba mpya United

Man united Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lingard akisaini mkataba mpya

Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard amesaini mkataba mpya na timu yake na atakua akivuna mshahara wa pauni 75,000 kwa wiki na kama watafuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya apata pauni 100,000 kwa Wiki.

Mkataba huo mpya utamuweka Jesse klabuni hapo mpaka mwaka 2021 na kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka moja zaidi katika mkataba huo wa sasa.

Lingard ameichezea klabu yake jumla ya michezo sabini, msimu huu amecheza michezo 29 na kufunga mabao 5 na alijiunga ma mashetani hao wekundu akiwa na miaka saba.

Mchezaji huyo alianza kuchomoza chini ya meneja Louis van Gaal na kabla ya hapo alipelekwa kwa mkopo kwenye Klabu za Leicester City, Birmingham City, Brighton na Derby County.