Maandamano ya kumtimua rais Zuma mamlakani yaanza

Maandamano ya kumng'oa mamlakani rais Zuma yaanza Afrika Kusini
Image caption Maandamano ya kumng'oa mamlakani rais Zuma yaanza Afrika Kusini

Maandamano ya kumpinga rais Jacob Zuma yameanza Afrika Kusini

Waandamanaji walikusanyika katika miji mikuu nchini humo wakitaka rais huyo kujiuzulu baada ya kufutwa kazi kwa waziri aliyeheshimiwa wa fedha.

Vikundi vya watu vilikusanyika kabla ya maandamano hayo katika miji ya Johannesburg, Cape Town, Durban na mji kuu wa Pretoria.

Hatua ya Zuma kumfuta kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan ilisababisha kukatwa kwa kiwango cha mkopo nchini humo.

Mwelekeo huo uliongezea shinikizo kwa uchumi wa Afrika Kusini ambao umekumbwa na utata.

Image caption Wamtaka rais Zuma kungatuka mamlakani

Maelfu ya watu walitarajiwa kuandamana na picha ambazo zilisambazwa katika mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa zikionyesha vikundi vikubwa vya watu nje ya bustani ya makanisa mjini Pretoria, ijapokuwa kulikuwa na hali ya ati ati ya iwapo maandamano hayo yalikuwa halali.

Polisi walisema siku ya Alhamisi kuwa maandamano mjini Pretoria sio halali kwasababu hawakuwa wamepewa kibali na mamlaka ya mji.

Lakini baadaye hatua hiyo ligeuzwa na hakimu.

Mijini Johannesburg, ambapo watu walikusanyika hatua chache kutoka makao makuu ya chama cha ANC, waendeshaji magari waliagizwa kutopitia katika maeneo ya biashara mjini humo.

Mamia ya wakongwe waliopigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na vijana walio wanachama wa chama kinachotawala walizingira nje ya makao makuu ili kulinda majengo yao.

Serikali ambayo ilitoa mwito wa amani wakati wa maandamano hayo yaliyofanyika nchi nzima, iliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa sharia za Afrika Kusini hulinda maslahi ya wote ikiwemo pia wale ambao hawakutaka kujiunga na maandamano.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maandamano dhidi ya Zuma Afrika Kusini

Mapema katika wiki, kamati ambayo hufanya maamuzi makubwa ndani ya chama cha ANC ilitupilia mbali malalamishi dhidi ya Zuma kuwa hakuwasiliana na watendaji wakuu kabla ya mabadiliko ya baraza la mawaziri.

Hatua ya kumng'atua Gordhan kutoka ofisi iliwakasirisha wanaompinga Zuma pamoja na wanaomuunga mkono, ikisababisha mgawanyiko ndani ya chama kinachotawala ANC, ambacho kimetawala Afrika Kusini kutoka mwaka wa 1994.

Iliwaacha baadhi ya viongozi wa ANC wakitia shaka iwapo Zuma anastahili kubaki kama rais.

Washirika wakuu wa ANC, chama cha South African Communist Party (SACP) na vyama vikuu vya wafanyikazi (Cosatu) waliunga mwito wake kutimuliwa.

Image caption Maandamano ya kumngatua mamlakani rais Zuma yafanyika katika miji yote Afrika Kusini

Lakini kamati ya chama (NWC), ikijadiliana kuhusu mabadiliko katika baraza la mawaziri, baadaye ilimuunga mkono rais.

Vyama vya upinzani, pamoja na washiriki wengine walio katika chama chake, walipanga maandamano ya siku ya Ijumaa kupitia maandamano ya umma kudai kujiuzulu kwake.Waandamanaji katika mji mkuu wanapanga kuandamana hadi makaazi ya serikali, katika majengo ya chama cha wafanyikazi