Wasanii waomba usaidizi wa kumtafuta Roma Mkatoliki
Huwezi kusikiliza tena

Wasanii waomba usaidizi wa kumtafuta Roma Mkatoliki

Wasanii nchini Tanzania kwa pamoja wametoa wito kwa vyombo vya dola sambamba na raia kusaidia kupatikana kwa msanii mwenzao Ibrahim Musa maarufu kama Roma Mkatoliki.

Hatua hii inakuja siku moja baada ya msanii huyo pamoja na wenzake watatu kukamatwa na watu wasiojulikana wakati wakiwa katika shughuli za kimuziki.

David Nkya na maelezo zaidi.