Serikali yaomba usaidizi kumtafuta Roma Mkatoliki

Msanii Roma Mkatoliki
Image caption Msanii Roma Mkatoliki

Serikali ya Tanzania imesema kwamba imepokea kwa mshutuko habari kuhusu kutoweka kwa msanii wa muziki Roma Mkatoliki.

Katika taarifa iliotiwa saini na kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Zawadi Msalia, wizara hiyo imesema kuwa imefuatilia kwa kina taarifa hiyo iliodai kuwa na mwelekeo wa Jinai.

Msanii Roma Mkatoliki ametoweka Tanzania

Huwezi kusikiliza tena
Wasanii waomba usaidizi wa kumtafuta Roma Mkatoliki

Imeongezea kuwa vyombo vya dola vimethibitisha kuwa msanii huyo hazuiliwi katika kituo chochote cha polisi.

Wizara hiyo sasa inawataka wadau mbali mbali na raia kutoa habari zozote kwa polisi zitakazosaidia kupatikana kwa msanii huyo.