Marekani kuimarisha biashara na China

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Markani Donald Trump Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Markani Donald Trump

Rais Trump wa Marekani na Rais wa Uchina, Xi Jinping, wamekubaliana juu ya mpango wa siku 100 ambapo mashauriano yatafanywa kati ya wawakilishi wa mataifa hayo jinsi ya kuimarisha biashara ya Marekani kwa Uchina ambapo bidhaa nyingi zaidi kutoka Marekani zitatarajiwa kuuzwa Uchina.

Akitangaza mpango huo muda mfupi baada ya Rais Trump kuwa mwenyeji wa mkutano kati ya viongozi hao wawili, Waziri wa biashara, William Ross alisema kuwa ingawa malengo yake ni ya kutia moyo; kwa ujumla kasi na mpango wa mashauriano kati ya mataifa hayo mawili yatabadilika.

Alisema mpango huo ni ishara kamili kuwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo muhimu kiuchumi duniani unazidi kuimarika.

Inadaiwa kuwa Bwana Trump alikubali mwaliko wa Bwana Xi kutembelea Uchina.

Naye Waziri wa mashauriano ya Kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, alisema kuwa Marekani itachukua hatua zake kibinafsi kukabiliana na mipango ya silaya za Korea Kaskazini, iwapo Uchina itasitasita katika hatua inazochukua.