Mahakama: Vipimo vya unywaji pombe havifai Kenya

Polisi wakimpima dereva wanayemshuku kunywa pombe Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wakimpima dereva wanayemshuku kunywa pombe

Wakenya sasa hawatashtakiwa tena kuhusu kiwango cha pombe walichokunywa baada ya mmiliki mmoja wa baa kudai kwamba vifaa hivyo vinaathiri biashara yake.

Kariuki Ruitha alilalama kwamba vifaa hivyo vinakiuka haki za wakenya kujifanyia uamuzi ikiwemo kiwango cha unywaji pombe.

Baadaya makabiliano ya miaka mitatu, mahakama ya rufaa ilitoia uamuzi uliompendelea.

Kenya ina barabara hatari duniani huku watu 1574 wakiripotiwa kufariki katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 pekee.

Wakiwa katika mahakama hiyo ya rufaa majaji hao watatu walisema kuwa madereva walevi wanaweza kushtakiwa chini ya sheria za trafiki ambapo kifaa hicho kinaweza kutumiwa.

Kulinga na ripoti za vyombo vya habari Bwana Ruitha ambaye anamiliki baa mjini Nairobi ,kwanza aliwasilisha kesi hiyo mahakamani miaka mitatu iliopita wakati alipomshitaki waziri wa uchukuzi.

Alikuwa amepoteza asilimia 80 ya biashara yake kwa sababu wateja wake walikuwa wakipimwa viwango vya pombe walivyokunywa wakati walipokuwa wakitoka hatua iliomlazimu kuwafuta kazi wafanyikazi 44 kulingana na gazeti la The Star.

Mwaka 2014,wakili wake alielezea sheria hiyo kuwa ya kiimla.

Hatahivyo ushindi wake huenda ukawa wa muda.

Majaji hao wameirudisha sheria hiyo bungeni ili kuandikwa upya.