Roma Mkatoliki na wenzake wapatikana Tanzania

Msanii Roma mkatoliki adaiwa kupatikana katika kituo kimoja cha polisi Jijini Dar Es Salaam Haki miliki ya picha Roma Mkatoliki
Image caption Msanii Roma mkatoliki adaiwa kupatikana katika kituo kimoja cha polisi Jijini Dar Es Salaam

Msanii Roma Mkatoliki aliyedaiwa kutoweka na watu wasiojulikana nchini Tanzania sasa amepatikana katika kituo cha polisi cha Oysterbay jijini Dar.

Habari hizo zimethibtishwa na mmiliki wa studio za Tongwe ambapo msanii huyo na wenzake wawili wanadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana siku ya Jumatano jioni.

Hata hivyo mmiliki huyo J Mada anasema kuwa hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi walipokuwa na ni akina nani aliokuwa wanawazuia.

Haki miliki ya picha Jamii Forums
Image caption Mtandao wa jamii forums

Mtandao wa Jamii Forums unasema kuwa kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa ukipaishwa na wasanii wenzake na mashabiki kuhusu kuachiliwa huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Serikali yaomba usaidizi kumtafuta Roma Mkatoliki

Awali, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishina Simon Sirro alisema bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea (kutekwa) kwa msanii Roma Mkatoliki na wenzake.