Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege futi 42,0000 angani

Wahudumu wa shirika la ndege la Uturuki wakiwa na mtoto aliyezaliwa Haki miliki ya picha Turkish Airlines
Image caption Wahudumu wa shirika la ndege la Uturuki wakiwa na mtoto aliyezaliwa

Wahudumua wa ndege ya shirika la ndege la Uturuki, walisherehekea kuwasili kwa abiria mwingine angani umbali ya futi 42,000 au mita 12,800, wakati mwanamke mmoja alijifungua mtoto msichana.

Abiria nao walisaidia kuzaliwa kwa mtoto huyo, muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji mkuu wa Guinea, Conakry, ikielekea Isanbul kupitia Burkina Faso.

Mama wa mtoto huyo aliyepewa jina Kadiju, walipelekwa hospitali wakati ndege hiyo aina ya Boeng 737 ilipotua mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.

Haki miliki ya picha Turkish Airlines
Image caption Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani
Haki miliki ya picha Turkish Airlines
Image caption Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani

Wote waliripotiwa kuchoka lakini walikuwa na afya nzuri.

Wahudumu waligundua kuwa mwanamke mmoja abiria kwa jina Nafi Diaby, alikuwa akihisi uchungu wa kujifungua.

Hapo ndipo walichukua hatua ya kumsaidia kujifungua ndege ikiwa safarini.

Mashirika mengi ya ndege huruhusu mama walio wajawazito wa hadi wiki 36 kusafiri, lakini uhitaji barua ya daktari wakifikisha wiki 28 kuonyesha tarehe wanayotarajia kujifungua.

Image caption Abiria ajifungua mtoto ndani ya ndege angani