Saudi Arabia kujenga mji mpya wa burudani karibu na Riyadh

Mji huo mpya utajengwa kando ya mji wa Riyadh Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mji huo mpya utajengwa kando ya mji wa Riyadh

Saudi Arabia imeanzisha mipango ya kujenga mji wa burudani kando mwa mji wa Riyadh ambao utakuwa mkubwa mara 50 zaidi ya himaya ya Uingereza ya Gibraltar.

Mji huo ambao utakuwa na ukubwa wa kilomita 334 mraba ambao utakuwa sawa na mji wa Las Vegas, utatoa huduma za kitamaduni, michezo na mambo mengine ya burudani.

Inaripotiwa kuwa mji utakuwa wa aina yake duniani.

Ujenzi wa mji huo utataanza mapema mwaka ujao na awamu ya kwanza kukamilika mwaka 2022.

Katika malengo ya mwaka 2030 uliotangazwa na naibu mfalme Mohammad Bin Salman mwaka mmoja ulipita, una lengo la kuboresha uchumi na kuzuia kutegemea mafuta kwa taifa hilo.

Mji huo ambao ni kama sehemu moja ya tano ya mji wa Riyadh, ndio mradi wa hivi punde kutangazwa.

Utawala unasema kuwa matumaini ni kuwa utawavutia wageni, kuboresha uchumi na ukawa wa burudani na furara kwa wale wataishi mji mkuu Riyadh.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mji huo mpya utajengwa kando ya mji wa Riyadh