Watu 13 wauawa kwenye mlipuko Mogadishu

Watu 13 wauawa kwenye mlipuko Mogadishu Haki miliki ya picha BBC WORLD SERVICE
Image caption Watu 13 wauawa kwenye mlipuko Mogadishu

Mlipuko wa gari katika kambi moja ya jeshi kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, umewaua takriban watu 13.

Ripoti zinasema kuwa mlipuaji aliyekua ndani ya gari iliyokuwa imejazwa milipuko, alijaribu kushambulia msafara uliokuwa ukimsafirisha mkuu wa jeshi la Somalia

Lakini badala yake gari hilo lilikumbana na gari lililokuwa limewabeba raia na kuwaua wote.

Haijulikani ni nani aliendesha shambulizi hilo lakini kundi la kislamu la al-Shabaab, mara nyingi limeshambulia maeneo kadha mjini Mogadishu.