Norway yatangaza mapambano dhidi ya ugaidi

Kifaa hicho kilikutwa katika sehemu iitwayo Gronland
Image caption Kifaa hicho kilikutwa katika sehemu iitwayo Gronland

Norway imetangaza kuwepo kwa mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi baada ya kugundua bomu lililotengenezwa nyumbani kwenye mji mkuu Oslo siku ya Jumamosi.

Kwa sasa imedhibitika kuwa ilipangwa kufanywa kwa shambulizi mjini hapo kama ilivyokuwa kwa miji ya nchi nyingine mfano Stockholm, St Petersburg na London iliyoteak siku za hivi karibuni.

Kijana wa miaka 17 raia wa Urusi amekamatwa akihusishwa na tukio hilo.

Mwanasheria wa kijana huyo anasema kuwa hizo ni njama tu.

Vyombo vya dola vinasema kuwa wamefanya mahojiano na kijana huyo na amekiri kuliunga mkono kundi la IS.