Wanasayansi wanasa picha ya nyota zilizogongana

Picha ya nyota changa zilizogongana Haki miliki ya picha ALMA (ESO/NAOJ/NRAO), J. BALLY/H. DRASS ET AL.
Image caption Picha ya nyota changa zilizogongana

Wanasayansi wamerekodi picha za kusisimua zinazoonyesha nyota mbili changa zikigongana na kuharibu mpangilio wao.

Nyota hizo ambazo ziko kwenye mkusanyiko wa Orion ziligongana miaka 500 iliyopita na kusababisha vumbi na gesi nyingi kuingia kwenye anga yao.

Wanasayansi wanasema kugongana kwao kulitoa nguvu kiasi kama cha zile zinazoweza kutolewa na jua kwa muda wa miaka milioni kumi.

Matukio yaliyojiri yamenakiliwa kwenye jarida la maumbile ya nyota.

Nyota hutengezwa wakati wingu kubwa la gesi linapoanza kusambaratika.

Kwa umbali wa miaka iliopita mwanga kutoka duniani, pamoja na nyota changa zilianza kuumbika katika wingu kubwa kwa jina Orion Molecular Cloud 1, (OMC - 1).

Mvuto ulileta nyota hizo karibu kwa kasi sana hadi miaka 500 iliyopita, huku mbili kati yazo zikigongana ana kwa ana na kusababisha mlipuko mkubwa uliosambaza gesi na vumbi katika anga kwa kasi kubwa.

Timu hiyo ya watafiti pia imegundua habari mpya kuhusu umbo la mwanga unaotokana na mlipuko huo.

Wanasanyasi hao wanajifunza kuhusu mgawanyiko na mwendo wa gesi ya kaboni iliyo kule ndani.

Hii itawawezesha kujua jinsi nyota inavyoumbwa.