Uchina kuwazawadi wanaowafichua majasusi wa kigeni

Uchina kuwalipa wanaowafichua majasusi wa kigeni Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Uchina kuwalipa wanaowafichua majasusi wa kigeni

Serikali ya China inatoa zawadi kubwa kwa wale ambao watatoa taarifa kuhusu kuwepo kwa majasusi wa kigeni.

Wakaazi wa mji mkuu wa China huenda wakalipwa hadi dola 72,000 kwa kutoa taarifa za siri.

Maafisa katika mji huo wanasema kuwa watu wanahitajika kusaidia katika "ujenzi wa ukuta wa chuma ya kukabiliana na maovu na kuchukua tahadhari dhidi ya majasusi".

Mamlaka zilizindua hamasisho mwaka uliopita , ikiwemo onyo dhidi ya kukukumbana na majasusi wa kigeni.

Utawala unasema kuwa mwezi Januari kundi la wavuvi kwenye mkoa wa Jiangsu walipata kifaa chenye majina ya kigeni wakivua samaki na kukisamma kwa mamlaka.

Kifaa hicho kiligunduliwa kuwa cha ujasusi kilichokuwa kikiichunguza China.