Pakistan yamhukumu kifo jasusi raia wa India

Pakistan yamhukumu kifo jasusi raia wa India Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pakistan yamhukumu kifo jasusi raia wa India

Mahakama moja ya kijeshi nchini Pakistan imemhukumu kifo aliyekuwa mwanajeshi mwanamaji raia wa India, ambaye alikamatwa mwaka uliopita na kufunguliwa mashtaka ya kupepeleza.

Kulbhushan Jadhav alikamatwa katika mkoa wa Balochistan na kulaumiwa kwa kuendesha shughuli za usaliti dhidi ya Pakistan.

Muda mfupi baada ya kukamatwa, Pakistan ilitoa video ambapo Jadhav, alionekana akikiri kushiriki katika upelelezi.

India inasema kuwa mwanamume huyo ni raia wake lakini imekana madai ya upelelezi.

Eneo la Balochistan limekumbwa na tatizo la ugaidi na Pakistan inaishutumu India kwa kuuunga mkono.

Pakistan inasema kuwa bwana Jadhav alikamatwa eneo hilo tarehe 3 mwezi Machi mwaka 2016.

India imelaani hukumu hiyo.

"Shri Jadhav alitekwa nyara mwaka uliopita kutoka nchini Iran na kuwepo kwake nchini Pakistan hakukuelezewa, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni ya India ilisema katika taarifa.