Ushahidi wa kashfa ya Shell, Nigeria

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nembo ya kampuni ya Mafuta ya Shell

Shirika la Habari la BBC, limepata ushahidi kuwa wakurugenzi wakuu katika kampuni ya mafuta ya Shell, walijua pesa zilizolipwa kwa serikali ya Nigeria, kwa maeneo makubwa ya visima vya mafuta, na kupitisjwa kwa mlanguzi wa fedha aliyepatikana na hatia.

Pia kulikuwa na sababu kuamini kuwa fedha hizo zingetumika kutoa hongo za kisiasa.

Mapatano hayo yalikamilishwa wakati ambapo kampuni ya Shell ilikuwa chini ya agizo la muda la kutofanya kazi kutokana na kesi ya ufisadi nchini Nigeria.

Kampuni ya mafuta ya Shell, inasema kwamba, haiamini kuwa wafanyikazi wake walikiuka sheria yoyote.

Kampuni hiyo kubwa ya mafuta duniani, imekuwa ikifanya kazi nchini Nigeria kwa karibu miaka 60, na ilikuwa imetazamia kupata kizima cha mafuta.

OPL 245 ni eneo rasmi la kisima cha mafuta nje kidogo tu ya pwani ya Nigeria, ambalo linakisiwa kuwa na zaidi ya mapipa milioni tisa ya mafuta, yenye kima cha dola nusu trilioni, kwa kiwango cha sasa cha kifedha.

Ushahidi huo mpya unaonyesha kuwa kampuni ya Shell, ilikuwa inapania kulitwaa.