China na Korea Kusini zimeionya kuiadhibu Pyongyang iwapo itarusha kombora lolote

Kombora la Korea Kaskazini, Tayari kufyatuliwa
Image caption Kombora la Korea Kaskazini, Tayari kufyatuliwa

Mataifa mawili ya bara Asia, yametoa onyo kali dhidi ya utawala wa Pyongyang, kwamba itaadhibiwa vikali, iwapo itadhubutu tena kufanyia majaribio zana zake za kinuklia.

Mataifa hayo, Korea Kusini na China, yamekiri kuchukua hatua kali dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwa tena itafanyia majaribio zana zake za kitonoradi zinazovuka mipaka ya kimataifa.

Tangazo hilo linatukia baada ya mkutano uliofanyika Seoul, kati ya wajumbe wa China na Korea Kusini, na hatua ya Marekani ya kutumameli za kivita hadi katika maeneo ya maji kwenye rasi ya Korea.

Taifa la Korea Kaskazini mara kwa mara limekuwa likiimarisha uwezo wake wa kivita, licha ya kuwekewa vikwazo na Umoja wa mataifa.

Kwa kweli, majaribio hayo ya mara kwa mara, yameongezeka sana chini ya utawala wa Rais Kim Jong-un.

Image caption Ramani ya Mataifa ya Bara Asia

Rais Trump wa Marekani, ameahidi "kutanzua" Korea Kaskazini bila ya kusaidiwa na China, mshirika wa pekee wa Pyongyang.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii