Sadio Mane kutocheza kwa miezi miwili

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mane aliumizwa goti lake la kushoto, baada ya kugongana na Leighton Baines kwenye mechi yao dhidi ya Everton

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, atafanyiwa operesheni ya goti siku ya Jumanne, na atakosa kusakata dimba msimu huu wote.

Aliumiza gegedu la goti lake la kushoto, baada ya kugongana na Leighton Baines kwenye mechi yao walioichezea katika uwanja wao wa nyumbani iyoishia 3-1 dhidi ya Everton.

Meneja Jurgen Klopp amesema kuwa Mane, mwenye umri wa miaka 25, anahitaji upasuaji, na kufanya kuwa "vigumu kwake kucheza msimu huu".

Timu ya Liverpool iko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Premia, huku ikisalia na mechi sita tu.

Haki miliki ya picha SADIOM ANEOFFICIAL
Image caption Sadio Mane aweka picha ya goti lake lililopata jeraha kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram

Jeraha hilo litamfanya kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili ijayo.

Mane alijiunga na klabu hiyo kwa kima cha Pauni milioni 34 kutoka timu ya Southampton msimu uliopita, na amesakata mechi zote sita za Liverpool msimu huu.

Katika mechi hizo, walishinda mchuano mmoja, tatu wakatoka sare na wakapoteza mechi mbili.