Bilionea wa magari Arnold Clark afariki akiwa na miaka 89

Mfanyibiashara huyo aliyezaliwa mjini Glasgow, alifungua biashara yake mwaka wa 1954.
Image caption Mfanyibiashara huyo aliyezaliwa mjini Glasgow, alifungua biashara yake mwaka wa 1954.

Bilionea muuza magari Arnold Clark, ambaye ni mwanzilishi wa kundi huru la kuuza magari nchini Uingereza amefariki akiwa na umri wa miaka 89.

Mfanyibiashara huyo aliyezaliwa mjini Glasgow, alifungua biashara yake mwaka wa 1954.

Taarifa ziliarifu kwamba alifariki kwa amani akiwa amezungukwa na familia yake.

Iliongezea kwamba Sir Arnold alikuwa mfano wa kuigwa na kwamba familia yake itaendelea kubeba maono yake.

Alidhibitishwa kama bilionea wa kwanza Uingereza aliyekuwa kwenye biashara za magari katika orodha ya matajiri katika gazeti la Sunday Times mwaka 2016.

Kampuni hiyo ambayo ina majina ya Sir Arnolds ina maduka 200 katika maeneo kadhaa Uingereza, ikiwa na zaidi ya magari 18,000 mapya na pia magari yaliotumika na kuwekeza faida ya puundi milioni 107.2 kwa mauzo ya paundi billioni 3.2

Taarifa kutoka kwa familia ilisema kuwa alifariki akiwa amezingirwa na familia.

Alikuwa bwana, baba na babu aliyependwa na rafiki mkubwa na mwajiri wa wengi.

Kampuni yake, Arnold Clark Automobiles, ilisema ilihuzunishwa kutangaza kifo cha mwanzilishi na mwenyekiti wake.