Miili ya watu 16 yapatikana Sudan Kusini

Vikosi vya serikali vinavyolinda amani sehemu hiyo
Maelezo ya picha,

Vikosi vya serikali vinavyolinda amani sehemu hiyo

Kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa huko Sudan Kusini kimesema kwamba kimeona miili ya watu waliokufa wapatao kumi na sita katika mji wa Wau.

Kiongozi rasmi wa waasi na padri mmoja wa kanisa katoliki kwa pamoja wameiambia BBC kwamba watu hao waliuawa kwa sababu ya misimamo yao ya kikabila.

Kiongozi huyo wa waasi Dominic Ukello, amesema kwamba vikosi vya serikali na wanamgambo washirika walikuwa wakiwalenga wanachama wa vikundi vya kikabila waliokuwa na mtazamo wa kuwaunga mkono waasi.

Na kueleza kwamba walikuwa wakijilipiza kisasi baada ya kushindwa kwa jeshi.

Kasisi Moses Peter, amesema kwamba raia wapatao elfu tano walikuwa wamekimbilia katika kanisa Katoliki huko Wau kuomba hifadhi kutokana na mauaji yanayoendelea .

Vikosi vya serikali vimekana kuhusika katika ghasia za kikabila, na kusema kwamba ghasia hizo zilifanywa na waasi na wanaowaunga mkono .