Huenda maafisa waliopanga shambulio la kemikali wakawekewa vikwazo.

Athari ya mashambulizi ya kemikali katika mji wa Khan Sheikhoun nchini Syria

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Athari ya mashambulizi ya kemikali katika mji wa Khan Sheikhoun nchini Syria

Mawaziri wa kigeni wa G7 watajaribu kuelewana kwa msingi mmoja kuhusu mashambulizi Syria, kabla ya katibu wa Marekani kuenda Urusi kujaribu kuishawishi kutoshirikiana na Syria.

Rex Tillerson pia atakutana na maafisa washirika wa nchi za mashariki ya kati kabla ya kwenda Moscow.

Uingereza ilipendekeza kutolewa kwa onyo la kuweka vikwazo vikali kwa Urusi na maafisa wa jeshi la Syria.

Mwelekeo huu unafuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya kemikali nchini Syria.

Syria imekana kuwa ilitimiza mashambulizi hayo ya kemikali katika mji wa Khan Sheikhoun unaoshikiliwa na waasi wiki iliyopita ambayo yaliwaua watu watu 89.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Jeshi la Syria limekashifu madai kutoka Marekani ya uharibifu mkubwa kwa kambi lao

Shirika la habari la Associated Press lilimnukuu afisa wa ngazi za juu Marekani akisema kuwa Warusi walifahamu shambulizi hilo la kemikali kwasababu ndege isiyokuwa na rubani ilikuwa ikizunguka hospitali moja mjini Khan Sheikhoun huku manusuru wakitafuta usaidizi.

Masaa chache baadaye ndege ilirusha makombora kwenye hospitali hiyo kwa kile kinachodhaniwa kuwa jaribio la kuficha shambulizi hilo.

Kwa mujibu wao Marekani ilisema iliharibu sehemu ya ndege iliyotumika na Urusi katika mashambulizi ya hewani katika kambi ya wanahewa wa Shayrat Alhamisi iliyopita huku mashambulizi zaidi yakitarajiwa.

Rais Trump na waziri mkuu wa Uingereza May walisema kwa njia ya simu kuwa sio mapendekezo ya Urusi kuendelea kumuunga mkono Rais Assad.

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa hivi sasa amekubaliana na rais Trump kuwa Rais Assad lazima awajibike.

Hata hivyo sera za Marekani kuhusu Syria hazijabainishwa kwa uwazi kwa wengi, huku Tillerson akisema kuwa hakujakuwepo mabadiliko ya kijeshi nchini Syria kufuatia mashambulizi ya angani ya Marekani na kwamba cha muhimu kwa Washington ni kuangamiza Islamic State (IS).