Kwa Picha: Jinsi wakimbizi Uganda wanavyopata maji

Mamia ya maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan kusini wamekimbia vita na njaa katika nchi yao na kutafuta usalama katika kambi zilizo kaskazini Uganda.

Zaidi ya wakimbizi 50,000 sasa wanaishi katika kambi ya Rhino ambayo imejaa vibanda na mahema karibu na mji wa Arua.

Maisha katika kambi hiyo ni ngumu, lakini wote wanakubaliana kuwa moja ya changamoto kali ni ukosefu wa maji.

Hamna mabwawa ya maji, na mito michache ambayo hupitia eneo hilo imekauka. Na kama haijakauka kabisa, maji yake ni kama matope.

Upande wa juu wa White Nile, Uganda Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Upande wa juu wa mto Nile, Uganda

Wakiongea kuhusu uhaba wa maji, shirika la msalaba mwekundu limeamua kusafirisha maji kutoka mto Nile, ambayo yanapimwa, yanatibiwa halafu yanapimwa tena kabla ya kuwekwa kwenye malori.

Baadaye yanaendeshwa yakipitia msituni hadi katika kambi, ambapo yanamiminwa ndani ya mamia ya matangi madogo, ambayo yanajazwa mara mbili au tatu kila siku.

Wakitumia mabomba na mashine kupandisha maji, maji huvutwa kutoka kwa mto hadi ndani ya matangi ambapo yanaongezewa kemikali ya aluminium sulphate ya kutoa masimbi.

Mradi huo ulioanza kutoa maji mapema mwezi huu, sasa umeajiri zaidi ya watu 40 kutoka nchini na mataifa ya kigeni.

Wakitumia mabomba, maji yanavutwa kutoka kwa mto hadi ndani ya tangi. Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Wakitumia mabomba, maji yanavutwa kutoka kwa mto hadi ndani ya tangi.
Mfanyikazi mmoja asimama kwenye ngazi katika mradi huo. Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Mfanyikazi mmoja asimama kwenye ngazi katika mradi huo.

Noor Pwani, mmoja wa wafanyikazi katika shirika la msalaba mwekundu alisema kuwa hiyo ndio njia pekee ambayo wangepambana na magonjwa ya kuambukiza, ambayo huleta wasiwasi mkubwa haswa ikizingatiwa hali duni ya mazingira katika kambi zilizojaa huku mvua ikitarajiwa kunyesha hivi karibuni ambapo huwa chanzo cha magonjwa yanayosababishwa na maji.

Agaba Derrick ambaye anafanya kazi ya kujitolea huwa na jukumu la kuangalia jinsi maji ya mto yalivyo.

Matokeo ya utafiti wake huamua kiwango cha aluminium sulphate kitakachoongezwa. Klorini pia huongezwa ili kuua bakteria waliobaki.

Mfanya kazi wa kujitolea, Agaba Derrick Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Mfanya kazi wa kujitolea, Agaba Derrick
A lab assistant weighs out a measure of chlorine powder Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption msaidizi wa maabara apima kiwango cha Chlorine

Wakati maji yanapotiririka upande mwingine, huonekana kuwa ni safi. Mradi huo unatayarishwa kutoa mamilioni ya lita ya maji kila siku.

Kiwango kinachotumiwa na mtu mmoja kila siku katika kambi ni kati la lita 15-20 ambayo hutumika kufua, kupika na kunywa.

Msafara wa malori takriban 30 husafirisha maji safi hadi maeneo ya usambazaji katika kambi, ambayo hujazwa mara tatu kila siku.

Katika maeneo mengine barabara ililazimika kukarabatiwa ili kuweza kustahimili malori kupitia hapo.

Maji yanapofunguliwa na kutoka upande wa pili huonekana kuwa safi. Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Maji yanapofunguliwa na kutoka upande wa pili huonekana kuwa safi.
Msafara wa takriban malori 30 husafirisha maji masafi hadi mahala pa kusambaza ndani ya kambi Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Msafara wa takriban malori 30 husafirisha maji masafi hadi mahala pa kusambaza ndani ya kambi
Wakaazi wa kambi ya Rhino wakisubiri katika eneo la kuteka maji na mitungi Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Wakaazi wa kambi ya Rhino wakisubiri katika eneo la kuteka maji na mitungi

Monica Achan, ambaye alitembea msituni kwa wiki mbili hadi Uganda baada ya shemeji yake kuuliwa na wanajeshi, anakunywa maji kutoka mto Nile katika makaazi yake mapya ndani ya kambi.

" Maisha ni magumu hapa, alisema. " Lakini tukiwa na maji tutaishi kwani maji ni uhai"

Monica Achan akinywa maji kutoka mto Nile Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Monica Achan akinywa maji kutoka mto Nile
Mwanamke ateka maji kutoka mfereji katika kambi ya Rhino Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Mwanamke ateka maji kutoka mfereji katika kambi ya Rhino
Msichana anatabasamu akiteka maji Haki miliki ya picha Tommy Trenchard / IFRC
Image caption Msichana anatabasamu akiteka maji

Picha na Ripoti na Tommy Trenchard.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii