Tiba ya seli ya ubongo, matumaini kwa ugonjwa wa kutetemeka

Tiba ya kutumia seli ya Ubongo, 'matumaini kwa ' kwa maradhi ya kutetemeka.

Chanzo cha picha, SPL

Maelezo ya picha,

Tiba ya kutumia seli ya Ubongo, 'matumaini kwa ' kwa maradhi ya kutetemeka.

Tiba ya kutumia seli ya Ubongo, 'matumaini kwa' kwa maradhi ya kutetemeka.

Wanasayansi wanaamini kuwa, wamepata namna ya kutibu na kukabiliana na maradhi ya kutetemeka maarufu Parkinson, kwa kurutubisha upya seli katika ubongo ulioharibika.

Wanasema kwamba seli katika ubongo wa binadamu inaweza kuchukuliwa na kujumuishwa ili kuchukua mahala pa ubongo ulioharibiwa na maradhi hayo.

Majaribio yaliyofanyiwa panya walio na dalili sawa na ule wa ugonjwa wa kusahau sahau, yanaonyesha kuwa tiba ya seli, inaweza kutuliza matatizo hayo.

Utafiti mwingi unafaa kufanywa kabla ya watu kuanza kufanyiwa majaribio.

Wataalamu wanasema kuwa, utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Nature Biotechnology unaleta matumaini makubwa, ingawa kwa sasa ni mwanzo mwanzo tu wa utafiti huo.

Wanasayansi wangali kuchunguza iwapo matibabu hayo ni salama, iwapo seli hizo zilizobadilishwa, ambayo huanza maishani kama astrocytes, zinaweza kufanya kazi, kama vile dopamine-nyuroni zinazopotea, mtu anaposhikwa na maradhi ya kutetemeka.