Trump kuiuzia Nigeria ndege za kukabiliana na Boko Haram

Ndege ya Super Tucano A-29 inaweza kutumiwa kwa ujasusi na kushambulia Haki miliki ya picha US Air Force
Image caption Ndege ya Super Tucano A-29 inaweza kutumiwa kwa upelelezi na kushambulia

Utawala wa Trump una mipango ya kuuza ndege za kivita kwa Nigeria licha ya kuwepo wasiwasi unaohusu ukiukaji wa haki za binadamu kufuatia shambulizi la ndege ambalo liliwaua raia kadha mwezi Januari.

Ndege kadha aina ya A-29 Super Tucano, zitauzwa kwa Nigeria kusaidia kulipiga vita kundi la kiislamu la Boko Haram, afisa mmoja wa Marekani alisema.

Makubaliano hayo ambayo hayathibitishwa rasmi yatahitaji kuidhinishwa na Congress.

Harakati za Boko Haram zimesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukimbia makwao.

Makubiano hayo yanayotajwa kuwa ya thamnai ya dola milioni 600 yaliafikiwa na utawala wa Obama, lakini yakakwama wakati yalistahili kupelekwa mbele ya Congress, baada ya kisa kibaya kilichowahusu wanajeshi wa Nigeria.

Karibu watu 90 wengi wanawake na watoto waliuawa mwezi Januari wakati ndege ya jeshi la Nigeria kimakosa, ilishambulia kambi iliyo kaskazini mashariki mwa nchi iliyokuwa ikiwahifadhi maefu ya watu waliokuwa wamewakimbia Boko Haram.

Shughuli ya ugavi wa chakula ilikuwa ikiendelea waakti wa shambulizi hilo.

Haki miliki ya picha Boko Haram video
Image caption Boko Haram wametangaza kutii kundi la Islamic State